Connect with us

News

Utepetevu Washuhudiwa Katika Wizara Ya Afya Huku Wakenya Wakichangia Vifo Kutokana Na Corona

Lamech Bwabi

Published

on

Hali ya wasiwasi imezidi kutanda nchini huku virusi vya corona vikisambaa kwa kasi sana.Visa vipya 605 vimeripotiwa nchini na kufikisha jumla ya idadi ya walioambukizwa kuwa 23,202.Shirika la afya duniani, (World Health Organization “WHO”) Ilisisitiza kuwa huenda mwezi wa tisa huenda ukawa kilele cha maambukizi ya corona nchini.
Idadi ya wanaopona pia inaongezeka ila wanaofariki pia wakiongezeka.Kutokana na utafiti wa hali ya shughuli hii inavyoendeshwa, imebainika kuwa kuongezeka kwa idadi ya wanaopimwa kunaongeza visa vya maambukizi na pia kuongezeka kwa idadi ya vifo.Waziri msaidizi msimamizi kwenye wizara ya afya Rashid Aman amedai kuwa hali ya anga imechangia kuongezeka kwa vifo.
Kulingana na Aman, msimu huu wa kipupwe(baridi kali) unazidisha maambukizi na hivyo kuchangia vifo.Kwa wiki moja sasa, idadi ya vifo imeonekana kupanda kwa kasi na wafanyikazi wa afya wakionekana kuathirika zaidi.Wa hivi majuzi ni muuguzi kutoka kwenye kaunti ya Homabay aliyefariki kule Kisii baada ya kusakamwa na virusi hivi akiwa na ujauzito.Mariam Owuor, muuguzi kwenye hospitali ya Rachuonyo alipiga moyo konde baada ya kuambukizwa virusi vya corona.
Utepetevu umeenea tangu Rais aiondoe nchi kwenye marufuku na hivyo basi kutishia hali ya afya ya mwananchi wa kawaida.Barakoa zimeonekana na kupatikana zimetapakaa kwenye maeneo ya umma na kuashiria jinsi uma umejilegeza kukabiliana na virusi hivi hatari vya corona.

Picha: Rais Uhuru Kenyatta Akihutubia

Huu si wakati wa visa vya ufisadi kuripotiwa ama wahudumu wa afya kugoma wakilalamikia marupurupu yao.Wauguzi kwenye kaunti ya Homa bay wanashiriki mgomo na kuathiri huduma zote za afya.Wanadai marupurupu yao tangu mwezi wa mei na kukosekana kwa vifaa vya kujikinga kutokana na virusi hivi hatari vya corona.
Licha ya kuwa masharti ya kutokusanyika mahali pamoja yangali, wakenya ni wale wale na shughuli zimerejea kawaida.Hawavai barakoa tena wakidai zinawafinya na hawapumui.Idadi ya vifo itazidi kuongezeka iwapo sampuli zaidi zitapimwa. Inavyobainika ni bayana kuwa virusi hivi vimo ndani ya jamii na iwapo idadi kubwa ya watu watapimwa(mass testing) basi wengi watakuwa kwenye hali ya wasiwasi.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Trending

%d bloggers like this: