Connect with us

Swahili News

Taifa Lililoathirika Zaidi Kutokana Na Virusi Vya COVID-19 Afrika Mashariki

Daniel Mutuva

Published

on

Tangu Kuripotiwa kwa Kisa Cha Kwanza Cha virusi vya covid-19, Mataifa Mengi yamekuwa yakikumbwa na janga hili hatari. China ndio inchi ya kwanza kuripoti kesi za covid-19 ambapo baadaye mataifa mengine Duniani yalianza kuripoti visa vingine.

Mataifa ya Bara la Afrika Ni miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na virusi hivi hatari. Taarifa zinabaini Kwamba virusi hivi ndio vimeanza kuathiri mataifa ya Afrika hasa Yale yaliyo na biashara za Hali ya juu yanayotembelewa na wageni Kutoka nche ya nchini.


Virusi hivi vya covid-19 vimekumba pia mataifa ya Afrika Mashariki. Serikali za mataifa haya imejaribu kuibua Mbinu mbalimbali kwa malengo ya Kudhibiti kuenea kwa virusi hivi. Mbinu mbalimbali zilizoibuliwa Ni pamoja na kuidhinisha Amri ya kutotoka nje katika masaa fulani, Kufunga Idara Mbalimbali pamoja na Kufunga taasisi zote za kielimu.

Aidha, Katika mataifa ya Afrika Mashariki, ripoti zinabaini Kwamba Kenya ndio mojawapo ya taifa ambalo limeathirika Zaidi na janga hili ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika Mashariki. Mataifa yanayohusisha Afrika Mashariki Ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Urundi.

Takwimu zinaonyesha Kwamba Kenya ndilo taifa linaloongoza kwa visa 5,206, Waliopona wakiwa 1823 na walioaga dunia 130. Kisha inafuatwa na Sudani Kusini na visa 1942, waliopona wakiwa 224 na walioaga dunia wakiwa 36.

READ ALSO:   Mishi Mboko: I Will Quit ODM If Raila Is Not On The Ballot

images-8
Taifa la tatu Ni Rwanda lililo na visa 830, huku idadi ya waliopona ikiwadia 376 na waliofariki wakiwa 2. Taifa la nne Ni Uganda lenye visa 805 na waliopona wakiwa 717 huku waliogada dunia bado hawajathibitishwa. Taifa linalofuata Ni la Tanzania likiwa na visa 509, huku takwimu ya waliopona bado haijaonyeshwa na walioaga dunia wakiwa 21.

Taifa la Mwisho lililo na visa chache vya virusi vya covid-19 Ni taifa la Urundi. Taarifa zinabaini Kwamba urudi imerekodi visa 144, huku waliopona wakiwa 93 na Aliyeaga dunia Akiwa Mmoja.

Toa Maoni, Shirikisha na Fuata Kwenye tovuti ya stateupdate.co.ke Kupokea Habari Zaidi.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Trending

%d bloggers like this: