Swahili News
Serikali Yatoa Agizo Kali Kwenye Sherehe Ya Mashujaa Siku Ya Jumanne

Siku ya Jumanne tarehe ishirini mwezi wa kumi taifa litaadhimisha sherehe za Mashujaa kwenye uwanja wa Gusii kule Kisii. Sherehe hizi huandaliwa kila mwaka kuwakumbuka na kuwatakia heri vigogo wale wote waliopigania Uhuru wa taifa hili. Pia watu mahiri ambao wametoa mchango mkubwa kwa manufaa ya taifa hutunukiwa. Sherehe za mwaka huu zitakuwa tofauti na miaka mingime kwani janga la corona limeikabili nchi na kutatiza mikutano mingi ya hadhara.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu maandalizi ya sherehe zenyewe, msemaji wa serikali kanali Cyrus Oguna amesema kuwa maandalizi yapo kabambe japo wote watakaohudhuria sherehe zenyewe watatakiwa kuvaa barakoa pamoja na kuzingatia masharti mengine ya kupambana na virusi hivi. Sherehe zitakuwa kwenye uwanja wa uma na hivyo basi watu wengi watahudhuria Rais wa taifa Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuongeza sherehe zenyewe.

Picha: Msemaji Wa Serikali Cyrus Oguna Kwenye hotuba ya awali
“Kinga ya kwanza ni yako binafsi, si ya serikali. Janga la corona lipo.”Alisema Oguna. Oguna amedai kuwa kuna baadhi ya watu wanaopuuza maagizo ya wizara ya afya na asilimia tisini ya wakenya kwa sasa hawavai barakoa. Kukaa kwa umbali wa mita moja unusu imekuwa jambo la kawaida na watu wanaandamana kwenye mikutano ya kisiasa na hata kukaa kwenye maeneo ya umma kwa karibu bila kujali ukali wa virusi vya corona.

Picha; Mkutano Wa Kisiasa Katika Kipindi Cha Janga la covid-19.
Oguna amewarai Wakenha kuchukua tahadhari kwani kinga ya kwanza ni wewe mwenyewe si kujikinga kwa sababu serikali imeagiza hivyo.Baadhi ya maagizo yaliyowekwa na wizara ya afya pamoja na serikali ni kuvaa barakoa, kukaa umbali wa mita moja unusu, kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni au kutumia viyeyuzi. Vyote hivo vitazingatiwa kwenye sherehe za kesho zitakazovutia wazalendo wengi.
Taifa limeendelea kurekodi idadi ya juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa siku tatu sasa ikipanda hadi asilimia kumi. Waziri wa afya Mutahi Kagwe ameonya kwamba huenda taifa linashuhudia msururu wa pili wa maambukizi na hivyo basi Wakenya wanastahili kuzingatia masharti yote ili kuzuia maambukizi zaidi.
Advertisements
-
News4 weeks ago
What Killed Tanzanian President John Magufuli
-
News4 weeks ago
Panic As Covid-19 Takes Two Family Members At The Same Time
-
News4 weeks ago
R.I.P Popular Royal Media Journalist Dies
-
World News1 week ago
Fearless Suluhu Reveals The Covid-19 Truth To Tanzanians, Overturns Magufuli’s Rules
-
Crime4 weeks ago
Tension: Heavily Armed Alshaabab Terrorists Take Over A Town
-
Health & Fitness3 weeks ago
Family Member Reveals Details On Raila’s Health
-
Politics3 weeks ago
R.I.P Ruto Thrown Into Deep Mourning
-
News3 weeks ago
Big Blow To Baba? How Uhuru Is Playing Raila In Favour Of Ruto