Connect with us

Swahili News

Serikali Matatani Baada Ya Waathiriwa Wa Virusi Vya Corona Kutishia Kuandamana

Dennis Avokoywa

Published

on

Huku awamu ya pili ya janga la virusi vya corona ikinukia humu nchini, waathiriwa wa virusi vya corona kaunti ya Kakamega wametishia kuandaa maandamano mjini Mumias wakilalamika kupokezwa huduma mbovu.

Waathiriwa hao waliopiga kambi katika kituo kimoja cha karantini eneo bunge la Mumias wanalalamika kuhangaishwa na madaktari wanaowahudumia wakiapa kuandaa maandamano hayo hadi kwa afisi za gavana kuwasilisha lawama zao.

Kulingana na waathiriwa hao ambao tumebana jina zao wanasema kwa kipindi cha zaidi ya siku 14 wamekuwa wakipiga kambi kwa kituo hicho na kunyimwa mahitaji yao ya kimsingi ikiwemo chakula na dawa.

“Tunakula mara mbili kwa siku. Chakula chenyewe kinaletwa saa kumi na moja jioni lakini mtapewa saa moji jioni ikiwa baridi.”

“Wanadai kutuhudumia kimatibabu ila hakuna dawa yoyote tunayopewa. Ukihisi maumivu popote unapewa antibiotix, hata kama ni maumivu ya kichwa,” akaongezea mwathiriwa mwingine.

Aidha wamelalamikia namna walivyosombwa na kupelekewakwenye kituo hicho wakitilia shauku vipimo wanavyopitishiwa, vipimo wanazosema huenda ndizo zimepelekwa wao kuambukizwa virusi hivyo.

“Maafisa wa afya walikuja kijijini mwetu na kutusomba bila hata kutupima. Walifanya hivyo baada ya mtu mmoja kijijini kufariki kutokana na virusi hivyo.”

READ ALSO:   Hatimaye Atakayemrithi Rais Kenyatta 2022 Abainika na Wala si Raila Odinga

“Unadungwa dungwa pua kila mara eti unapimwa, huenda kudungwa huko ndiko kutuambukiza virusi hivyo, tutaandamana kulalamikia hii.” Akasema mwathiriwa mwingine.

Ni semi zilizokinzana na za katibu mkuu wa muungano wa wauguzi kaunti hiyo Renson Bulunya ambaye pia ni mmoja kati ya waasiriwa kwenye karantini hiyo akikanusha madai hayo na kusema huduma mule ndani ni za kuridhisha japo kuna uhaba wa madaktari.

“Hapa hulazimishwi kuja. Kabla ya kuletwa lazima upimwe na wadhihirishe unaugua virusi hivyo”. Akasema.

“Tunakumbwa na uhba wa madaktari kutokana na idadi ya waathiriwa inayozidi kukuwa kila kuchao”. Akaongezea Bulunya.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya kaunti ya kakamega ilikuwa imeandikisha zaidi ya waathriwa 400 kufikia tarehe 6 Novemba idadi hiyo ikihofiwa kuongezeaka hata zaidi iwapo waathiriwa hao wataandaa maandano na kutangamana na watu wengine.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: