Connect with us

Swahili News

Sababu Zitakazofanya Shule Kufungwa Tena Licha Ya Kufunguliwa

Daniel Mutuva

Published

on

Picha; Wanafunzi wa Shule Ya Umoja darasani

Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha alibaini Kwamba Punde tu virusi Vya covid-19 vitakavyopungua nchini, basi ufunguzi Wa shule utapewa kipau mbele. Hii ilitokea Baada ya taasisi zote za kielimu Kufungwa ili Kukabiliana na kutapakaa kwa virusi hivyo hatari.

Aidha, Wizara ya Elimu ikishirikiana na Serikali ya Kenya, iliamua kuangazia ufunguzi wa taasisi za kielimu ila chini ya amri Kali. Wizara ya Elimu ilibaini kwamba itafungua shule kwa msingi Wa kufuata kanuni za virusi Vya covid-19. Ufunguzi Wa shule ulianza kwa awamu, huku wanafunzi wa mwaka wa mwisho wanaokamilisha masomo yao ya viwango mbalimbali kupewa kipau mbele.

Picha: Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha

Katika hatua iliyochukuliwa,wanafunzi wa vyuo vikuu walipaswa kurudi shuleni Tarehe 5 mwezi huu huku wanafunzi wa daraja la 4, darasa la nane na kidato Cha nne kurudi Tarehe 12 mwezi huu. Wizara ya Elimu imeshakwisha kutoa kalenda ya masomo Jinsi na namna masomo yatakavyoendelezwa Katika maadalizi ya mitihani ya kimataifa.

 

Aidha, Waziri Magoha alisisitiza kwamba, iwapo shule imefungua na haijazingatia kanuni za Kudhibiti Kusambaa kwa covid-19, basi hakuna budi Ila kuifunga Tena. Kufuatia na ripoti za hivi Karibuni, Rais Uhuru Kenyatta alikariri kwamba tusiangalie lini shule zitafunguliwa Ila Ni namna tutakavyofungua shule.

READ ALSO:   Sad News Over Schools Reopening in 2021 As Controversial Details Emerges

Wizara ya Elimu ilikuwa imebainisha shule kufunguliwa mwaka Ujao januari. Kusisitiza, Katika hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta ya hivi Karibuni, alibaini Kwamba ikiwa shule zitafunguliwa mwaka Ujao, ni vyema basi ikiwa zimezingatia kanuni za kuzuia kutapakaa kwa covid-19. Kila taasisi ya Elimu iliombwa na wizara ya Elimu chini ya uongozi Wa Waziri Prof George Magoha kuhakikisha wamefanya maandalizi kapambe Katika kanuni za Kudhibiti Kusambaa kwa covid-19 shuleni.

Aidha, Katika pitapita Zake za kikazi, Waziri Magoha alibaini Kwamba taasisi nyingi za kielimu bado hazijatimiza kanuni za covid-19. Magoha aliamrisha Kwamba taasisi hizo za kielimu zitasalia Kufungwa Hadi Wakati zitakapotimiza kanuni za covid-19. Na zile Ambazo zitaenda kinyume na kanuni hizo, zitafungwa Tena.

Toa Maoni, Shirikisha Na Fuata Kupokea Habari zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: