Sababu Zitakazofanya Kutoisha Kwa Virusi Vya Covid-19 Nchini Kenya Hivi Karibuni

0
112 views
PICHA: Wahudumu Wa Afya Wakijiandaa kushughulikia wagonjwa wa covid-19

Tangu Kuripotiwa kwa kesi Cha kwanza Cha virusi vya covid-19 Katika mji wa Wuhan, Taifa la china, mataifa mengi duniani yamekuwa yakikumbwa na janga hili kwa kiasi kikubwa. Taarifa zinabaini Kwamba uchumi wa mataifa mengi duniani umezoroteka Huku wengi wakipoteza Kazi walizokua wanazifanya apo awali kwa ajili ya kujipatia riziki ya kila siku. Takwimu zinabaini Kwamba idadi ya walioambukizwa na virusi vya covid-19 duniani imetimia takribani 7, 458, 993, katika kesi hizi, zilizohai ni 3,261, 749. Walioaga dunia ni takribani 419,020 na idadi ya waliopona ni 3,778,224.

Aidha, nchi ya Kenya Ni miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na janga la virusi vya covid-19. Serikali ya Kenya ikishirikiana na shirika la Afya Duniani WHO, limekuwa likijitahidi kwa kuzua Mbinu mbalimbali kuzuia Kuenea kwa virusi hivi hatari licha ya Kwamba inazidi kupata Pigo Kali.

PICHA: Wahudumu Wa Afya Wakishughulikia wagonjwa wa covid-19

Tangia kuchibuka kwa virusi hivi, Kenya imerekodi kesi 3,094 Huku idadi ya Kifo ikitimia 89 na waliopona wakiwa 1,048.
Kulingana na taarifa, Baadhi Ya wakenya hawafuati Sheria na taratibu zilizoidhinishwa na Serikali kwa ajili ya kuzuia kutapakaa kwa virusi hivi nchini. Wengi hususia taratibu hizi na hatimaye kuchangia kuongezeka kwa idadi ya kesi za covid-19. Kuna baadhi ya mambo ambayo yataweza Kuchangia katika kuongezeka kwa virusi hivi nchini. Kutovalia barakoa, kutonawa mikono kwa Kutumia kitakaza Mikono, kutoheshimu Sheria ya kutotangamana na watu, kutotunza usafi na kadhalika.

Taarifa zinabaini Kwamba Kenya bado iko Katika Hali ya kukabiliwa vikali na janga hili la covid-19, tatizo Kubwa likiwa kutotii Sheria kwa Wakenya wengi. Hivi majuzi Raisi Uhuru Kenyatta alikuwa ametangaza kutoa kufuli na kikwazo cha kurudi nyumbani mapema mnamo June 6 2020 na wakenya wengi walionekana wakisherehekea lakini hali ikawa sivyo. Rais Uhuru aliongeza vikwazo kwa kipindi cha siku 30 mbele.

READ ALSO:   No Burial Permit Without Covid-19 Certificate-Mutua
PICHA: Rais Uhuru Kenyatta akihutubia Taifa kufuatana na Janga la covid-19

Ni wazi Kwamba, Wakenya wengi hawajali maisha yao wala ya wenzio. Ni Ishara Kwamba wakipewa uhuru, Kenya itaoza, wengi watakumbwa na ndwele hii Hali ambayo itapelekea idadi ya vifo kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Toa Maoni, Shirikisha Na Fuata Kwa Kubonyeza Kengele Nyekundi Chini Kushoto Kupokea Habari Zaidi.

Advertisements
Advertisements

Leave a Reply