Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kubadilishwa kwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC. Tume hii imekuwa ikishtumiwa na kutiwa doa tangu kura za mwaka wa 2017 ambapo mahakama ya juu iligutilia mbali kura za urais ikidai kuwa hakukuwa na wazi jinsi ahughuli yote ya uchaguzi iliendeshwa. Baadhi ya makamiahna kama Chiloba wakasimamishwa kazi, Akombe akajiuzulu na Msando akauwawa.
Viongozi hasa kutoka upinzani wamekuwa wakishinikiza mageuzi kwenye tume hii kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Inavyoonekana ni kwamba baadhi ya watu wamepoteza imani kwa tume hii na wanaamini kuwa haiwezi andaa uchaguzi mwingine kwa njia ya haki.Imesalia tu miaka miwili kabla uchaguzi mkuu ujao na pia kunatarajiwa kura ya maamuzi karibuni kupitisha mapendekezo ya BBI.
Ruto amekuwa akimsuta kinara wa ODM Raila Odinga na wandani wake kwa kuilaumu time ya IEBC kila anapopoteza uchaguzi. Kwenye baadhi ya mikutano yake, Ruto alisema kuwa hata wakitaka wamweke kakake Raila, Oburu Odinga kama mwenyekiti yeye haogopi kwani wananchi ndio wanaamua ni nani wanataka awaingoze.
Miezi michache iliyopita, aliibua madai kuwa kuna watu wanapanga kuiba kura na kumzuia kuongoza taifa hili. Kwenye uzinduzi wa BBI, Ruto alisema kiwa yeye hapingi mageuzi kwenye tume hiyo bali anataka usawa. Alipeana mfano wa timu za mpira wa soka baadhi kumchagua mwamuzi itasababisha mchezo usiwe wa haki. Alicho maanisha ni kuwa vyama vyote vihusishwe katika kuwachagua makamishna hao.
Msukosuko huu unaashiria kuwa hata iwapo uchaguzi utafanyika leo, wale watakaoahindwa watailaumu tume ya IEBC.Kutiliwa doa kwake kumesababisha baadhi ya watu kukosa imani nayo na hivyo basi ni wakati mwafaka viongozi wa taifa waketi chini na kutatua shida hii.