Connect with us

Swahili News

Rais Kenyatta Taabani Baada Ya Naibu Wake Ruto Kutoboa Siri

Daniel Mutuva

Published

on

Picha: Naibu Rais William Ruto

Matamshi ya Naibu Rais William Ruto yaonekana kutia Rais Kenyatta Taabani kutokana na kutofaulisha agenda kuu nne za jubilee alizozitaja Rais Uhuru. Hali hii ilitokana Baada ya Naibu Rais William Ruto kumsuta hadharani Gavana Wa Kakamega Wycliffe Oparanya pale Bungoma.

 

Akizungumza Katika mahudhurio ya mazishi ya mwendazake Maurice Mambonga Wanjala, babake mbunge Mwambu Mabonga hapo Jana 26 Disemba 2020, Naibu Rais alimsuta Gavana Oparanya kwa Kukosa kushughulikia matatizo yanayowakumba watu wa eneo la magharibi mwa Kenya.

 

Hata hivyo Gavana Oparanya alisema Kwamba wamefanya kila juhudi kuwasilisha ripoti kuhusiana na kufufuliwa kwa viwanda vya sukari eneo hilo la magharibi lakini uongozi wa jubilee umeshindwa kutekeleza ombi lao.

 

“Tulifanya mikutano kadhaa juu ya kufufuliwa kwa viwanda vya sukari Magharibi mwa Kenya na tumewasilisha ripoti yetu lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa, “alilaumu Oparanya

Aidha, Gavana Oparanya ambaye Ni Naibu Mwenyekiti wa Chama Cha ODM na Mwenyekiti wa Baraza la magavana, alidai kwamba Kaunti hazijapata fedha Kutoka kwa hazina kwa muda wa mwezi ambazo zinatumika  kuendelesha shughuli za Kaunti.

 

“Wengine wetu hawawezi kwenda katika ofisi zetu kwa sababu hatujalipa wakandarasi kati ya huduma zingine kwa sababu ya ukosefu wa fedha, ”oparanga aliongeza

READ ALSO:   Ukipendwa Pendeka! Alfred Mutua Launches A Multimillion Hotel Named After His Lover (Photos)

 

Akijibu madai ya Gavana Oparanya, Naibu Rais William Ruto alisema kwamba ripoti ya BBI ndio imetinga agenda za maendeleo ya Serikali ya Jubilee. Alidai kwamba timu ya BBI ambayo inajumuisha Gavana Oparanya ilikuja kwao na kuwataarifu kwamba Kuna Jambo la dharura linalohitaji kutatuliwa na ndio sababu agenda ya maendeleo ya Jubilee pamoja na utekelezaji wa mpango wa kufufua viwanda vya sukari imeachwa.

 

Picha: Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya

“Timu ya BBI ambayo ni pamoja na Oparanya ilikuja na kutuambia kwamba kuna dharura ambayo inahitajika kutatuliwa. “Ndiyo sababu ajenda ya maendeleo ya Jubilee ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa kufufua viwanda vya sukari imeachwa,” Naibu Rais alisema

 

Naibu Rais pia aliongeza Kwamba agenda kuu nne za Serikali ya Jubilee Ambazo zilikuwa zinanuia kubadilisha maisha ya Wakenya zimewekwa pembeni kutokana na maendeleo ya Kisiasa ya hivi karibuni.

 

Ajenda Kuu Nne zimewekwa pembeni , kwa sababu sasa lengo zaidi ni BBI, agenda hizi zilikuwa na lengo la kushughulikia masuala muhimu yanayoathiri Wakenya, ”Ruto alibainisha.

Fuata Kwenye tovuti Stateupdate.co.ke Kupokea Habari zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Trending

%d bloggers like this: