Pigo Kwa Ruto Baada Ya Wandani Wake Kumhepa Hadharani, Raila-Uhuru Washerehekea

0
244 views

KWA MUHTASARI;


  • Naibu Rais ahepwa na Wandani Wake na Kuunga mkono mswada wa BBI.
  • Watano hao walijitokeza Hadharani bungeni na kupiga kura ya uungaji wa mswada wa BBI huku wenzao TangaTanga wakionekana kupinga kwa kiasi Kikubwa.
  • Aidha, Wandani hao wa Naibu Rais Ruto wajitetea kwa kauli kwamba uamuzi huo si wao binafsi bali Ni wananchi waliowachagua.

Stateupdate Swahili na Daniel Mutuva


KWA  UPANA; 

Naibu Rais William Ruto apata pigo kali Baada ya Wandani Wake Kumhepa Hadharani. Wandani hao watato wameonekana kuunga mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu Wa Zamani Raila Odinga. Taarifa zinaibuka kutokana na shughuli za upigaji kura kwa kuunga au kupinga mswada wa BBI uliofanyika bungeni.

 

Mswada wa BBI umekumbana na upizani Mkubwa kutoka kwa mrengo wa Ruto unaojulikana Kama TangaTanga huku wafuasi wake wakitupilia mbali mswada huu na kuwakashifu waungaji wake Hadharani. Wabunge si haba walijitokeza bungeni na kuunga mkono mswada wa BBI hususan kutoka mrengo wa Kieleweke wanaoegemea upande wa Rais Kenyatta na Bwana Odinga.

 

Aidha, Licha ya Upinzani uliokita mizizi kutoka kwa Mrengo wa Naibu Rais kuhusu mchakato wa BBI, Ruto apigwa butwaa Baada ya Wandani Wake kubadili mkondo Hadharani.

READ ALSO:   Itumbi Leaks Details On DP Ruto's Ongoing Meeting At His Residence in Karen

 

Baadhi ya Wabunge wa TangaTanga walijitokeza bungeni na Kuunga mkono mswada wa BBI Wakati wa shughuli za upigaji kura. Wandani hao Ni pamoja na Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri, Mbunge mteule David Ole Sankok, Mbunge wa Maara Kareke Mbiuki, Mbunge wa Mugirango kaskazini Joash Nyamoko na Mbunge wa Njoro Purity Kathambi.

Picha; Mbunge Wa Bahati Kimani Ngunjiri akihutubia Katika shughuli ya awali

Watano hao wamehepa uamuzi wa TangaTanga na Kupasua mbarika na kuwaacha wenzao kinywa wazi.
Akizungumza Baada ya kufanikisha mchakato wa BBI, Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri alidai Kwamba bado yumo ndani ya TangaTanga na uamuzi wa uungaji mkono BBI ulitokana na watu wa Bahati na wala si maamuzi yake binafsi.

 

Akisuta madai ya Mbunge wa Suna Mashariki na Kiongozi wa wachache bungeni Mohammed, Ngunjiri amedai Kwamba TangaTanga bado haijafariki na iko imara hadi uchaguzi Mkuu mnamo 2022.

Fuata Kwenye tovuti stateupdate.co.ke Kupokea Habari zaidi.

Advertisements
Advertisements

Leave a Reply