Connect with us

Swahili News

Pigo Kwa Ruto Baada Ya Rais Kenyatta Kubaini Mkondo Wa Ruto Hadharani

Daniel Mutuva

Published

on

Picha; Naibu Rais William Ruto

Naibu Rais William Ruto apokea Pigo Baada ya Rais Uhuru Kenyatta kumsuta hadharani katika Ukumbi wa Bomas Katika Uzinduzi rasm wa ripoti ya BBI. Ripoti hii ilipokezwa kwa Rais Kenyatta na Waziri Mkuu Wa Zamani Raila Odinga Katika Kaunti ya Kisii siku moja Baada ya sherehe ya Mashujaa Katika uwanja wa Michezo wa Gusii.

Aidha, Akihutubia Katika Ukumbi wa Bomas hapo Jana, Rais Kenyatta waliomba viongozi kuunga Mkono ripoti ya BBI ili Kufanikisha Kazi kwa pamoja. Rais, alisisitiza Kwamba Katika Miaka ya nyuma, nchi ya Kenya imekuwa ikikumbwa na Vita vinavyoibuka kutokana na tofauti za Uchaguzi Mkuu. Rais Uhuru alibaini Kwamba ripoti ya BBI inakadiria kuwaleta Wakenya Wote pamoja na kutatua utofauti unakumba wakenya kwa pamoja.

Picha; Naibu Rais William Ruto (Kushoto), Rais Uhuru Kenyatta (Kati) na Waziri Mkuu Wa Zamani Raila Odinga (kulia) Katika Uzinduzi rasm wa Ripoti ya BBI Katika Ukumbi wa Bomas mnamo 26, Oktoba 2020

 

Akimsuta Naibu Rais William Ruto, Rais Kenyatta alimkanya Ruto kwa mwendo wake Wa Kasi wa Kisiasa unaoibua utofauti. Hii Ni Baada ya Naibu Rais na Wandani Wake wamekuwa wakipinga ripoti ya BBI na kukosoa Waziri Mkuu Wa Zamani Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta chini ya Madai Kwamba ripoti ya BBI inanuia kutenga nafasi za viogonzi Wa juu huku ikitenga wengine na mwananchi Wa kawaida.

Picha: Rais Uhuru Kenyatta (Kushoto) na Raila Odinga (kulia) wakibeba ripoti ya BBI Katika Kaunti ya Kisii

 

READ ALSO:   Revealed! Did Aden Duale Receive Pornographic Materials When With Family?

Rais Kenyatta alimshukuru Naibu Rais Ruto kwa kusonga naye Katika Upande wa Chama Cha jubilee hadi Mambo yalipoenda kombo Wakati Ruto alianza siasa za kuwania Urais Mnamo 2022 akasahau kujihusisha na kazi. Rais Kenyatta alifananisha uongozi wa urais Kama Mbio za wanaspoti ambapo Mmoja anapokeza kijiti kwa mwenzake kuendelea na Mbio kwenda mbele. Hata hivyo, Rais Kenyatta alibaini Kwamba badala ya kuenda mbele, Naibu Rais Ruto amepinduka na kuenda nyuma.

 

Namshukuru DP upande wa Jubilee kwa sababu tulisonga pamoja.Hapa katikati ndio 2022 ikaanza…akasahau yale mengine…Ndio maana nasema tutulize ball…Hii race ni relay. Lakini sasa hapa my brother William anapinduka anakimbia nyuma…Mos mos tutafika tu,” Rais Uhuru Kenyatta alisema

Toa Maoni, Shirikisha na Fuata Kupata Habari Zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: