Connect with us

Education

Namna Waziri Magoha Ajipata Taabani Kwa Kufungua Shule

Lamech Bwabi

Published

on

Waziri wa elimu profesa George Magoha alitangaza kufunguliwa kwa shule kwa awamu baada ya visa vya maambukizi vya virusi hatari vya corona kupungua.Mwanzo, waziri huyo aliagiza kufunguliwa kwa vyuo vikuu hasa wanafunzi waliokiwa kwenye mwaka wao wa mwisho na wiki moja baadae wanafunzi wa kidato cha nne, darasa la nane, na nne kufuata mtawalia. Hii ni chini ya masharti makali ya kuvaa barakoa na idara hizo za elimu kuhakikisha kuna maji ya kutosha na viyeyuzi ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo iwapo vingekuwepo shuleni.
Mambo yanaonekana kuchukua mkondo mwingine kwani tena idadi ya maambukizi inazidi kupanda kila uchao. Katibu msimamizi kwenye wizara ya afya Dr. Rashid Aman, kwenye mazungumzo ya kila siku akitoa takwimu alisema kiwa visa vya maambukizi vimeanza kupanda na kupita ile asilimia ya tano. Ikumbukwe kuwa shirika la afya Ulimwenguni (WHO) ilitoa mwongozo kuwa taifa likiripoti visa vya maambukizi chini ya asilimia tano, basi shughuli zake za kawaida zaweza rejelewa.
Inavyoonekana, ni kuwa taifa limeanza kuripoti awamu mpya ya maambukizi ya virusi hivi. Dr. Aman alidai kuwa iwapo maambukizi yatazidi kupanda itabidi shule zimefungwa tena maadamu maisha ya wanafunzi yatakuwa hatarini.Baadhi ya wazazi wameelezea kughadhabishwa kwao na hatua ya Profesa Magoha kufungua skuli na hata kadha wamekataa kuwaruhusu watoto wao kwenda shuleni. Rais alikiwa amesema kuwa shule hazitofunguliwa karibbuni lakini waziri huyo wa afya alishikilia msimamo wake na kutaka masomo yarejelewe.
Wakenya wanazidi kumponda waziri Magoha kwenye mitandao ya kijamii huku wakimlaumu kufanya uamizi wa haraka. Iwapo maambukizi yataendelea kupanda itamlazimu rais kuchukua hatua kali ili kudhibiti usambaaji wa visa hivi. Hii itajumuisha kufungwa tena kwa shule hadi virusi hivi vikabiliwe.
Waziri Magoha alisisitiza kuwa Walimu wakuu kwenye shule za umma na kibinafsi wasiwatume wanafunzi nyumbani kwa kukosa karo. Wazo hili pia limeibua hisia mseto miongoni mwa walimu wakishangazwa na Waziri kwani bila karo wafanyikazi na hata walimu watalipwa aje pasi na karo. Hii inaonekana kudidimiza viwango vya elimu kwani walimu wanahitaji kula na kulala ili wazidi kujitolea kwenye kazi zao.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: