Namna Wanafunzi Wengi Wamepotoka Kimaadili Nyumbani Katika Kipindi Hiki Cha Covid-19.

0
135 views
PICHA: Mwanafunzi Wa Shule ya Umoja anayevuta sigara

Kwa muujibu wa utafiti wa kina uliotekelezwa hivi Karibuni, wanafunzi wengi wamepotoka Kimaadili nyumbani Baada ya shule kufungwa ili kupambana na kutapakaa kwa virusi vya Covid-19. Hivi Karibuni Serikali ilifunga taasisi zote za kielimu kutokana na janga hili la virusi vya corona ambalo limeathiri mataifa mengi duniani. Wanafunzi walilazimiswa kukatiza masomo yao na kurejea Nyumba.

Kufuatana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni, Wanafunzi Wengi huchukua muda wao mwingi kuzurura mtaani bila la Kufanya Licha ya Kwamba Serikali ilibaini Kwamba wanafunzi Wote Nchini Kenya watapokea mafunzo yanayopeperushwa moja kwa moja Kupitia vyombo vya habari. Aidha, Wengi wao hujiusisha na masuala hasi Katika jamii. Wengi wao wanajiusisha na unywaji wa pombe, usinzi, utumiaji Wa madawa ya kulevya na kadhalika.

 

PICHA: Wanafunzi Wa shule ya Upili waliokamatwa wakitumia madawa ya kulevya

Taarifa Zaidi zinabaini Kwamba akina dada Wamo Katika Hali ya Hatari. Wengi wao wamepachikwa mimba bila mpango ilihali bado wachanga. Serikali imeombwa kuangazia suala hili kwa kuzua vikwazo ikishirikiana na walinda vijiji kuhakikisha Kwamba suala hili limekomeshwa daima. Kulingana na utafiti, Wengi wa wanafunzi hujiusisha na masuala haya bila umakinifu. Yahitaji tuungane pamoja tukomesha hulka hii inayoibuka miongoni mwa wanafunzi Katika jamii Katika Kipindi Hiki mataifa mengi duniani yanajikaza na kupambana na Virusi Vya Covid-19. Hawa Ndio kizazi kijao na chaitaji kutunzwa.

Advertisements
Advertisements

Leave a Reply