Connect with us

Politics

Namna Raila Ameichanganya Jamii Ya Mlembe

Lamech Bwabi

Published

on

Eneo la magharibi limegawanywa na kugeuzwa ngome ya wageni. Tangu kifo cja aliyekuwa makamu wa Rais wa Kenya Michael Kijana Wamalwa, Jamii ya Mulembe imeshindwa kupanda mchongoma ili kupata kiti cha juu cha Urais. Miaka nenda miaka rudi, jamii hiyo imekuwa ikimuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga kama alivyodokeza kinara wa ANC Musalia Mudavadi.

Wito wa baadhi ya wakazi na viongozi wa eneo hilo kubuni chama kimoja umesambaratika na umezikwa kwenye kaburi la sahau. Mapinduzi kwenye chama cha Ford Kenya tena yanakadiriwa kwenye ANC yameigawanya jamii ya Luhya. Mmoja wa kinara wa NASA, Wetangula amepoteza wadhifa wake na hivyo kushusha matumaini yake kabisa na chama.

PICHA; Musalia Mudavadi 

Weta amemlaumu Raila kwa yanayoshuhudiwa eneo la magharibi na amemtaka kinara huyo kuiwacha jamii ya Mulembe. Mkutano ulioandaliwa nyumbani pa katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli, ulizua tumbo joto na sasa mipango yake inaonekana.
Mkutano huo ulihudhiriwa na wabunge, maseneta, magavana na hata waziri Eugene. Gavana wa Kakamega alitwikwa jukumu pamoja na Atwoli ya kuiongoza jamii hiyo kisiasa ili kurudisha hadhi ya eneo hilo. Baada ya mkutano huo, chama cha ODM kilifanya mageuzi kwenye mabaraza mbalimbali ya bunge na wengi wa wabunge kutoka eneo la magharibi waliathirika kwa kuwa washirika wa karibu wa Naibu wa Rais.

READ ALSO:   Prepare For Tough Days Ahead, Uhuru's Govt Announces Strict Measures

Naibu kiranja wa wachache Chris Wamalwa alipoteza kiti chake kilichonyakuliwa na Eseli Simiyu mbunge wa Tongaren. Hali hii ikasababisha tena msukomsuko ndani yachama cha Ford Kenya ambapo Chris aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa chama na Eseli kutemwa. Huu ndio ulikuwa mwanzo na mwisho wa Weta kwani Eseli pamoja na Wafula Wamunyinyi walifanikisha kumbandua kama kinara wa chama hicho.

Toa Maoni, Shirikisha, Na Fuata Kwenye tovuti stateupdate.co.ke Kupata Habari Zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: