Connect with us

Politics

Namna Matiang’i Anavyotatiza Azma Ya Ruto Kuwa Rais

Lamech Bwabi

Published

on

Nafasi ya Naibu wa Rais Dr William Samoei Arap Ruto kwenye serikali inazidi kuibua maswali mengi kwani anavyoongea na kutekeleza majukumu yake basi hakai kuwa ndiye wa pili kwenye uongozi. Uhusiano wake na kiongozi wa taifa Rais Kenyatta ulitibuka na hivyo kusababisha yeye kufanywa kama mgeni kwenye serikali ambayo anaiongoza. Hata wendani wake kama Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kupitia ukurasa wake wa twitter alifanya utani kwa kuweka picha ya Matiang’i akimkaribisha Rais na kuandika kuwa naibu wa Rais Fred Matiang’i atamkaribisha rais.
Ni bayana kama tundu kuwa Ruto ndiye Naibu wa rais kikatiba ila uhusiano mbaya na rais ndio unafanya aonekane kama aliyepotea. Hivi karibuni kumechipuka uhasama baina ya Matiang’i na wandani wake naibu Rais. Amekashifiwa kwa masaibu yanayomkumba naibu kiongozi huyo wa Jubilee na kushtumiwa kwa kulemaza shughuli zake zote.
Photo: Naibu wa Rais William Ruto, Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na Rais Uhuru Kenyatta wakiwa wanashiliki mazungumzo
Wiki iliyopita mikutano kadhaa iliyopangwa na Ruto ilitibuliwa na maafisa wa kulinda usalama wakisema kuwa ni agizo kutoka ngazi za juu. Ruto amekuwa akiendeleza uhamasisho wa kuwainua akina mama na boda boda na pia kuchangia kanisani kwenye sehemu mbalimbali za taifa. Safari zake hizi zimewavutia wengi na wakati mmoja rabsha zilizuka kule Muranga ambapo watu wawili walipoteza maisha yao. Matiang’i alitetea hatua hiyo ya kufutilia mkutano wa Nyamira lakini hakisazwa na wandani wake rais.
Mbunge wa Kiharu Ndidi Nyoro aliropokwa na hata kumtaka waziri hiyo wa usalama kumtia mbaroni kwa kuhudhuria mkutano huo kile Nyamira siku ya Alhamisi.Mikutano hiyo ya kisiasa imegeuka uwanja wa kutupiana cheche na kulaumiana kwani kila mwamba ngoma huvuta kwake.
Uongozi wa Rais Kenyatta umemfanya Matiang’i kuwa kigogo wa kisiasa kwani ameongezewa majukumu na kila yakiongezwa uhasama unapanuliwa baina yake na naibu wa rais. Waziri huyo mwenye msimamo mkali huenda akawania kiti cha ugavana kuke Nyamira kama inavyodaiwa na baadhi ya wachambuzi wa maswala ya kisiasa.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: