Home News Crime Namna Filamu Za Ngono Zimeathiri Wanafunzi Wengi Nyumbani Huku Visa Vya Ujauzito Vikiongezeka

Namna Filamu Za Ngono Zimeathiri Wanafunzi Wengi Nyumbani Huku Visa Vya Ujauzito Vikiongezeka

0
Namna Filamu Za Ngono Zimeathiri Wanafunzi Wengi Nyumbani Huku Visa Vya Ujauzito Vikiongezeka

Ni Suala la kustaajabisha namna wanafunzi Wengi wameathirika nyumani Licha ya taasisi za elimu Kufungwa kukabiliana na uthibitishaji wa virusi vya covid-19 nchini. Taarifa zinabaini ya Kwamba wanafunzi Wengi wamepotoka kimaadili Hali Ambayo imechangia pakubwa kuathirika kwao. Wengi hawatunzi maadili yanayohitajikana katika jamii huku wakitenda mengi kwa uamuzi wao binafsi.

Hivi majuzi, takwimu za visa vya ujauzito mwiongoni mwa wanafunzi wa kike nchini zilitolewa. Huku Kaunti ya Machakos ikiangaziwa, ripoti zilibaini Kwamba takribani wanafunzi 4000 wamepachikwa mimba. Hata hivyo, ripoti zaidi zilionyesha Kwamba wanafunzi 200 hupachikwa mimba kila wiki katika Kaunti ya Machakos.


Kulingana na utafiti wa kina uliofanywa kuhusiana na suala hili, ilibainika Kwamba mitandao ya kijamii imechangia pakubwa katika upunguaji maadili mwiongoni mwa wanafunzi, hali Ambayo imesababisha visa vya ujauzito kati ya wanafunzi kuongezeka. Filamu za ngono wanaotizama wanafunzi nyumbani katika kipindi hiki cha covid-19 zimeathiri wanafunzi wa kike kwa kiasi kikubwa.

Ripoti Zaidi zinathibitisha Kwamba, wanafunzi wakitizama Filamu hizo za ngono huwa wanakuwa na ilhamu ya kujaribu na wenzao Wa kiume au watu na wengine. Pia mtazamo huo huibua hisia mwiongoni mwao za kutaka kushiriki katika Mchezo huo mchafu.

READ ALSO:   The Shocking Rate Of Teenage Pregnancy During Covid-19 Calls For Action

Kulingana na ripoti za hivi karibuni, Kuna Baadhi za vipindi wanavyotizama wanafunzi Kwenye Runinga ambavyo huchangia kudidimia kwa maadili miongoni mwao. Kwa mfano, Kipindi Cha Uigizaji Cha Maria kinachopeperushwa katika Runinga ya Citizen, Kimetambulika kuathiri maadili miongoni mwa wanafunzi licha ya Kwamba kinaandamana na mafunzo pia na Baadhi ya madili yanayoitajika katika jamii.

Ni jukumu la wazazi kuhakikisha Kwamba wanadhibiti watoto wao wakiwa Nyumbani. Imebainika Kwamba wanafunzi Wengi huzurura mtaani hata Baada ya Serikali kutanga Kwamba wanafunzi wanapaswa kusoma wakiwa Nyumbani wakingoja shule kufunguliwa.

Toa maoni, Shirikisha na Fuata katika tovuti ya stateupdate.co.ke kupata habari zaidi

Advertisements
Advertisements

Leave a Reply

%d bloggers like this: