Connect with us

Swahili News

Mwanaume Kakamega Apokezwa Kichapo Cha Mbwa Kwa Kukwepa Bila Kulipa Pesa ya Lodgi

Dennis Avokoywa

Published

on

Mwanaume Kakamega apokezwa kichapo cha mbwa kwa kukwepa bila kulipa pesa ya lodgi

Inaripotiwa kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 34 alimshawishi binti mmoja mjini humo kushiriki naye tendo la ngono akiahidi kumlipa shilingi 300 pesa alizotaka kupunguziwa kwa kisingizio ya gharama ya juu ya maisha.

Kwa kukosa hela hizo alikata shauri ya kutoroka kwenye chumba walimokuwa wamelala kabla ya kufwatwa na msichana huyo aliyemkamata na kuziraruwa nguo zake akianika uchi wake mbele ya umati wa watu.

“Nataka pesa zangu, nataka pesa zangu, baada ya kujitosheleza kwangu unataka kuniacha kama kiraka”.

“Nitakuaibisha kwa kurarua nguo zako na kuanika uchi wako mbele ya rafiki zako”. Akaahidi binti huyo.

Kulingana na walioshuhudia kihoja hicho walisema ni hulka ya mshukiwa huyo kuwalaghai mabinti mjini humo na baada ya kujitosheleza kingono yeye huwakwepa.

“Hakuwa na lolote la kumlipa. Alitumia pesa zote kununuwa vinywaji walizokunywa kabla ya kupishana misuli. Ni tabia yake kuwatumia wasichana na kuwakwepa”. Akasema mkaazi mmoja.

Hata hivyo mwanaume huyo alipokezwa kichapo cha mbwa na wakaazi hao hii ikiwa ni funzo kwa wale wenye hulka ya kuwatumia mabinti kingono kabla ya kumlipia pesa hizo wakimwonya dhidi ya kurudia kitendo hicho.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: