Swahili News
Mwanaume Afariki Wakishindana kubugia Pombe

Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Emukangu wadi ya Shirere viungani mwa mji wa Kakamega baada ya mwanaume mmoja eneo hilo kufariki kwa madai ya kubugia pombe kupita kiasi.
Mwendazake alikuwa na wenzake wawili kwenye mashidano ya kubugia pombe aina ya changaa ambapo mshindi angetuzwa kwa kununuliwa pombe wiki nzima.
Kulingana na wagemaji walioshuhudia kisa hicho wanasema aliyefariki ni Juma Salim Mwale, 45 huku wenzake Godfrey Mushira na George Shivachi wakinusurika kifo baada ya kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kakamega wakiwa hali mbaya.
“Watatu hao walifika kwa kituo hiki cha changaa wakiwa tiyari wamelewa. Mmoja wao aliwanunulia pombe na kwa pamoja wakaanza kushindana atakayebugia zaidi, mshindi akiahidiwa kununuliwa pombe wiki nzima.” Akasema Morris Mboyi
“Mwendazake alibugia vikombe vitano na kufariki papo hapo huku wenzake wakiokolewa walipokuwa kwa kikombe cha tatu kila mmoja na kukimbizwa kwa hospitali ya rufaa ya Kakamega.” Akaongezea mgemaji mwingine.
Akidhibitisha kufariki kwa mwendazake, naibu chifu wa Shirere Fanice Atsienza amewaonya wakaazi dhidi ya kubugia pombe kupita kiasi.
“Pombe bila chakula ni hatari kwa maisha yako. Unywaji wa pombe kupita kiasi inauwa.” Akasema.
Aidha ameinyoshea kidole cha lawama idara ya mahakama kwa kile alidai ni wao kutowajibika ipasavyo kwani kila wanapowakamata wanaoendeleza biashara hiyo haramu na kuwapeleka mahakamani, wao huwachiliwa kwa njia zisizoeleweka.
“Atazuiliwa kwa masaa machache kabla ya kurejea kwa biashara yake haramu,” akaongezea Atsienza.
Ni tukio lililokashifiwa vikali na wakaazi eneo hilo wakihusisha kufunguliwa kwa maeneo ya burudani na vilabu kama chanzo cha watu kulewa kupindukia na kukiuka maagizo ya wizara ya afya kudhibiti msambao wa virusi vya corona wakitaka maeneo yote ya burudani kufungwa.
-
News4 weeks ago
What Killed Tanzanian President John Magufuli
-
News4 weeks ago
Panic As Covid-19 Takes Two Family Members At The Same Time
-
News4 weeks ago
R.I.P Popular Royal Media Journalist Dies
-
World News1 week ago
Fearless Suluhu Reveals The Covid-19 Truth To Tanzanians, Overturns Magufuli’s Rules
-
Crime4 weeks ago
Tension: Heavily Armed Alshaabab Terrorists Take Over A Town
-
Health & Fitness3 weeks ago
Family Member Reveals Details On Raila’s Health
-
Politics3 weeks ago
R.I.P Ruto Thrown Into Deep Mourning
-
News3 weeks ago
Big Blow To Baba? How Uhuru Is Playing Raila In Favour Of Ruto