Connect with us

Politics

Matukio Yanayotarajiwa Kabla Ya Uchaguzi Ujao

Lamech Bwabi

Published

on

Siasa za kumrithi Rais Kenyatta zimeshika kasi hata kabla tume ya uchaguzi haijatangaza kuanza kwa kampeni rasmi. Ni miaka miwili kabla ya Kenyatta kukamilisha hatamu yake ya miaka kumi kama Rais wa nne wa taifa la Kenya. Uongozi wake ulitarajiwa kuwa bora zaidi na kuendeleza kile alichoanzisha mwanzilishi wake Rais Mstaafu Mwai Kibaki lakini imebainika kuwa mambo hayakamilika.
Tangu Jubilee ilipochukia hatamu chini ya Rais Kenyatta na Naibu wake Ruto, Wakenya walikuwa wenye matumaini chingu nzima maadamu viongozi hao ni wenye umri mchanga na hivyo kuwa wachapakazi. Kitumbua kiliingia mchanga tangu kinara wa ODM alipohusishwa kwenye juhudi za mapatano na mpango mzima wa BBI kubuniwa. Huu umekuwa uongozi ambao Rais na Maibu wake hawafanyi kazi kama kitu kimoja na hivyo basi kukata matumaini ya Wakenya.
Hii ni ishara tosha kwamba uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa aina yake na matukio na matokeo mbalimbali yatashamiri vyombo vya habari.
 
Cheche za maneno/ Kauli kinzani
Hili lishaanza kwani Naibu wa Rais na aliyekuwa Waziri mkuu wameonekana mara si moja wakibadilishana maneno makali kwenye ziara zao za kisiasa. Siasa zinapozidi kushika kasi, wanasiasa wanajiunga na mirengo mipya na hivyobkutoa kauli za kukejeli wapinzani wao.Cheche hizi zaweza kutishia usalama wa taifa kwa kuwa baadhi ya wanasiasa wenye ubinafsi wanatumia wananchi kusambaratisha taifa na kutaka kuzua machafuko. Siasa za chuki zilipitwa na wakati na taifa limepiga hatua hivyo basi matokeo ya mwaka wa 2007 hayafai kujirudia.
Mirengo mipya/ Kusambaratika kwa vyama
Wanasiasa wana uhuru wa kuhama toka chama kimoja hadi kingine iwapo wanahisi haki zao zinakandamizwa ama wanaona hawatapata nafaai bora ya kiwa kwenye debe.Kabla ya uchaguzi mkuu ujao, kuna wale washabaini fika kwamba wakiridi kwenye debe kutumia tiketi ya chama waliyotumia awali hawatapita kwa kiwa matendo yao yamekuwa yakupigania chama kingine.
Vyama na miungano ya sasa vitafikia kikomo na vingine vipya kutengenezwa.
Kwa mfano mmoja wa Kinara alidai kuwa NASA ilishasambaratika na wakati wake utakapotimia basi mkataba utaisha na vyama tanzu kung’atuka. Pia kutokana na maururu wa mivutano kwenye chama tawala, ni wazi kwamba Jubilee itavunjika au baadhi ya vinara kujitoa na kuunda muungano au chama kingine.
Kampeni kutwa kucha
Jinsi siku zinavyozidi kusonga ndivyo upinzani wa kisiasa unashika kasi. Kampeni zishaanza na zitaendelea kila siku kwa kasi hasi uchaguzi ukamilike.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: