Connect with us

Health & Fitness

Mapuuza Ya Wakenya Yatachangia Mlipuko Wa Pili Wa Corona

Lamech Bwabi

Published

on

Hali ya wasiwasi imerejea nchini baada ya taifa kurekodi visa vya juu tena ya virusi hatari vya corona. Kama alivyotangaza waziri msimamizi kwenye wizara ya afya Dr Raahid Aman, huenda Kenya inashuhudia msururu mpya wa maambukizi kama mataifa mwngine ya kile ulaya. Idadi ya maambukizi ilikuwa imepungua chini ya asilimia tano na kupelekea rais kulegeza baadhi ya masharti na hata baadhi ya wanafunzi kurejea shuleni. Sasa idadi hiyo imepanda hadi asilimia kumi na huenda nchi ikatakiwa kuwa tena chini ya masharti.
Utepetevu na ulegevu wa Wakenya ndio chanzo cha kuongezeka kwa visa hivi vilivyokuwa vimepungua. Tangu rais aisndoe masharti makali, watu wamesahau kuvalia barakoa na kurejelea hali ya kawaida. Hapo awali, idara za usalama zilikuwa zinawaadhibu wale wasii na barakoa na hata ikawa nadra na adimu mtu kuingia kwenye maeneo ya umma bila barakoa. Lakini sasa watu wanatembea hohehahe wasivae hata barakoa kwenye kidevu kama ilivyokuwa awali.
Mikutano ya kisiasa ni kama imerejelewa. Viongozi mbalimbali wamekuwa wakihudhuria makongamano na hata kufanya kampeni ambapo watu wengi walihudhuria mikutano yenyewe. Umbali wa mita moja na nusu hauzingatiwi tena na hata kuna wale wenye magonjwa miongoni mwao na hawachukui hatua ya kuwalinda wenzao. Kwenye mikutano hii iwapo mtu mmoja ameambukizwa virusi hivi, vitasambaa kwa haraka na kushika wengi wa Wakenya haswa wenye mapuuza.
Kuna baadhi ya wale wanaodai kwamba virusi hivi havipo kwa kuwa hawajamwona wala kukutana na hata mhasiriwa mmoja aliyeambukizwa. Tahadhari kabla hatari na majuto ni mjukuu huja kinyume. Isiwe kwamba kwa sababu virusi havipo kwenye eneo lako basi havipo, corona ipo na ni hatari kama alivyotangaza waziri wa afya Mutahi Kagwe. Mapuuza haya ndio yamepelekea kutoisha kwa virusi hivi.
Mojawapo ya masharti kutoka kwa wizara ya afya ili kujikinga corona ilkuwa kuosha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka ama kutumia viyeyuzi. Pia kupimwa kwa joto mwilini na kutafuta matibabu iwapo dalili zisizo za kawaida zitajitokeza. Ni watu wachache tu wanaozingatia hili wengine wanaishi kwenye falsafa za kale kwamba wao ni Waafrika.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: