Connect with us

Swahili News

Kilichosababisha Kifo Cha Gavana Nyagarama Chabainika Na Wala Si Covid-19; Familia Yatetea

Daniel Mutuva

Published

on

Picha: Gavana Wa Nyamira Mwendazake John Obiero Nyagarama

Huku huzunu ukiendelea kutanda katika Kaunti ya Nyamira kutokana na Kifo Cha Gavana John Obiero Nyagarama, taarifa zimeibuka kubaini kiini halisi kilichosababisha Kifo Cha mwendazake.

 

Inabainika Kwamba Gavana Nyagarama alilazwa Katika hospitali ya Nairobi Baada ya Kuambukizwa virusi Vya covid-19. Siku ya jumapili Nyagarama alilazwa Katika chumba Cha wagonjwa mahututi kutokana na kulemewa kwa hali yake ya kiafya.

 

 

Aidha, familia ya mwendazake Gavana Nyagarama imebaini kiini halisi kilichosababisha Kifo chake. Kulingana na ripoti, familia ilitaja Kwamba alipata shida ya kupumua baada ya mapafu yake kuanguka.

 

 

Hata hivo, Nyagarama alikuwa akipambana na Ugonjwa wa shinikizo la damu kwa muda mrefu ambapo alikuwa akipokea matibabu kila mwezi. Wakiibua hisia zao mbalimbali, Wakaazi wa Nyamira wamemtaja mwendazake Nyagarama Kama Kiongozi aliyekuwa shupavu na Mwenye maendeleo aliyenuia kuzua maendeleo Katika Kaunti ya Nyamira.

 

Picha: Gavana John Nyagarama Akihutubia hapo awali

Viongozi mbalimbali nchini wametuma rambirambi zao kwa familia na wakaanzi wa Nyamira kwa ujumla. Walioomboleza Kifo chake Ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, Naibu Rais William Ruto, Waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matiang’i na wengineo.

READ ALSO:   Revealed: The Exact Amount Of Money The Government Spends Weekly To Help Vulnerable Families Amid Covid-19

 

 

Hali hii imetokea kutokana na ongezeko la virusi Vya covid-19 linaloshuhudiwa nchini huku visa vya wanaoambukizwa vikizidi kuongezeka. Hali hii ilizuia kusafiri ngambo kwa wanasiasa Kupokea matibabu kutokana na vikwazo.

 

 

Tangu kuriporiwa kwa kisa Cha kwanza ya Ugonjwa huu nchini Mnamo Machi 2020, Kenya imerekodi visa 93,405 huku idadi ya waliopona ikitimia 74,999 na walioaga dunia wakiwa 1,618. Aidha Serikali ikishirikiana na wizara ya Afya na mashirika mengine ya kiafya imeibua mbinu mbalimbali kuzuia kuenea Zaidi kwa virusi hivi hatari.

Tembelea tovuti Stateupdate.co.ke Kupokea Habari zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: