Swahili News
Kifo! Mwanamke Azuiliwa kwa madai ya kumuwa Mwanawe wa kiume

Maafisa wa polisi wa kituo cha Navakholo, kaunti ya Kakamega wanamzuilia mwanamke mmoja eneo hilo kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuuwa mwanawe wa miaka 7.
Irene khayasi, anadaiwa kumpiga David Wafula kichwani mara kadhaa kwa kutumia kifaa butu baada ya mwendazake kukosa kukamilisha kazi aliyokuwa amewachiwa kuifanya.
Mwendazake alitakiwa kukamilisha kazi ya kuosha vyombo pamoja na kufua nguo zake kabla ya mamake kurejea akitoka kwenye hafla moja ya mazishi, kijiji jirani.
Kulingana na waakazi walioshuhudia kisa hicho, wanasema mshukiwa amekuwa akimdhulumu mwendazake kwa kumpiga mara kwa mara huku juhudi zao kujaribu kumkanya zikiambulia patupu.
“Si mara ya kwanza mwendazake kucharazwa na mshukiwa. Ipo siku alimpiga hadi akamvunja mkono kwa kosa dogo tu.”
“Alitakiwa kukamilisha kazi ya usafi nyumbani kabla mamake kurejea akitoka kwa hafla moja ya matanga kijiji jirani.” Akasema mkaazi mmmoja.
Akidhibitisha kisa hicho, naibu chifu wa shinoyi josphat mutinye amesema mtoto huyo alifariki alipofikishwa hospitalini kutokana na majeraha mabaya aliyopokezwa na mamake.
“Alimpiga hadi akaziria. Nilifahamishwa tukio hilo kupitia kwa wenyeji. Tulifanya mpango wa kumkimbiza hospitalini ila alidhibitishwa kaaga akiwa njiani.” Akasema Mutinye.
Aidha mutinye amewaonya wazazi dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi kila wanapowaadhibu wanao akisema mshukiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa shtaka la mauaji.
-
News3 weeks ago
What Killed Tanzanian President John Magufuli
-
News3 weeks ago
Panic As Covid-19 Takes Two Family Members At The Same Time
-
News4 weeks ago
R.I.P Popular Royal Media Journalist Dies
-
Health & Fitness4 weeks ago
Sad News To Kenyans On NHIF After A Major Development
-
World News5 days ago
Fearless Suluhu Reveals The Covid-19 Truth To Tanzanians, Overturns Magufuli’s Rules
-
News4 weeks ago
Good News To Kenyans As Medics Leaks Health Condition Of Raila in Isolation
-
Crime4 weeks ago
Tension: Heavily Armed Alshaabab Terrorists Take Over A Town
-
Health & Fitness3 weeks ago
Family Member Reveals Details On Raila’s Health