Connect with us

Swahili News

Hofu Yatanda Baada Ya Msemaji Wa Serikali Kuambukizwa Homa Kali Ya Corona

Lamech Bwabi

Published

on

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amedhibitishwa kuambukizwa virusi hatari vya corona.Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wake rasmi wa tweeter, Oguna amesema kuwa alipimimwa virusi vya covid baada ya kuonyesha dalili zinazoambatana na homa hiyo kali ya mapafu.Alisema kuwa matokeo yalitoka na kuonyesha kuwa ameambukizwa homa hiyo.
“Recently having come from an assignment outside town,I developed mild corona  virus related symptoms and got tested.The results came back positive for corona virus and I am now receiving medical and responding well to treatment at an isolation and treatment facility.Contact tracing is ongoing and my family is OK.I urge all Kenyansto take the disease seriously and take all necessary precautions to avoid getting infected. #komeshaCorona.”

Picha; Msemaji Wa Serikali Cyrus Oguna

Hivi karibuni baada ya kutokea kwenye majukumu viungani mwa jiji, nilionyesha dalili za virusi vya corona na nikapimwa.Matokeo yalikuwa chanya na sasa napokea matibabu kwenye kituo kimoja cha kutengwa.Shughuli ya kutafuta niliotangamana nao inaendelea na familia yangu ipo salama.Nawasihi wakenya wote kuchukulia maradhi haya kwa uzito na wajikinge ili wajizuie kutoambukizwa.Aliandika Oguna.
Hali yake ya afya imekuwa kwenye hatihati baada ya majuzi kudaiwa kuwa kanali huyo mstaafu ameambukizwa homa hiyo.Oguna kupitia akaunti yake ya tweeter alikana madai hayo na kusema kuwa hali yake i shwari.Alifutilia uvumi wote kwenye mitandao uliokuwa ukisema kuwa ameambukizwa homa hiyo kali ya mapafu alipokuwa jijini.
Wakenya hawakusita kurejelea kauli hiyo ya Oguna baada ya kuposti tena akisema kuwa ameambukizwa homa hiyo.Kumekuwa na tetesi pia kuwa waziri wa maswala ya ndani ya nchi Fred Matiang’i ameambukizwa homa hiyo inayotatiza dunia nzima.Ilidaiwa kuwa Matiang’i amelazwa kwenye hospitali ya Aga Khan anakopokea matibabu.
Hata hivyo, wizara hiyo kupitia mtandao wake imefutilia mbali uvumi huo na kusema kuwa waziri huyo yu buheri wa afya.Uvumi huo umechangiwa na kunyamaza kwa waziri huo wakati huu ambapo swala la usalama linapaswa kuoewa kipau mbele has marufuku ya kutotoka nabkuoatikana nje(curfew).
Wakenya wamekuwa wenye mapuuza na sasa baada ya matokeo haya kutoka kwenye ikulu, ni ishara kuwa ugonjwa upo na unaweza shika mtu yeyote.Wizara ya afya inakusihi kuvaa barakoa, kuzingatia usafi na kukaa nyumbani ili uwe salama na tuangamize corona.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Trending

%d bloggers like this: