Home Lifestyle Health & Fitness Hii Ndio Hospitali Inayoendeleza Huduma Zake Za Kawaida Licha Ya Covid-19; Ripoti Zabaini

Hii Ndio Hospitali Inayoendeleza Huduma Zake Za Kawaida Licha Ya Covid-19; Ripoti Zabaini

0
Hii Ndio Hospitali Inayoendeleza Huduma Zake Za Kawaida Licha Ya Covid-19; Ripoti Zabaini

Kutokana na virusi Vya covid-19 nchini Kenya, Baadhi ya hosiptali nchini zimeregeza huduma zao za kawaida na kutilia mkazo katika kushughulikia virusi Vya covid-19. Kenya Ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika na Janga hili huku idadi ya visa vya covid-19 inchini vikizidi kuongezeka. Ripoti zabaini Kenya Sasa imerekodi visa 8,067 tangu kuchipuka kwa virusi hivi hatari.

Aidha, katika mahojiano ya Asubuhi Kwenye runinga ya NTV Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kenyatta Daktari Kamuri amebaini Kwamba Licha ya Janga hili ambalo limesababisha baadhi ya Hospitali zingine kuregeza huduma zao za kawaida, hospitali ya Kenyatta ndio Hospitali Pekee inayoendeleza huduma Zake za kawaida Kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizungumza, daktari Kamuri alimfahamisha mwanahabari Gradys Gachanja kwamba hospitali ya Kenyatta haikusimamisha huduma Zake za kawaida Licha ya covid-19. Daktari Kamari alibaini Kuwa huduma za kliniki zaendelezwa kawaida na kunao takribani wagojwa 1800 katika Wadi wanaohudumiwa kutokana na magonjwa tofauti.

Picha; Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kenyatta Daktari Kamuri

“Hospitali ya Kenyatta ni hospitali pekee ambayo haikuacha kutoa huduma baada ya COVID-19. Kliniki zinafanya kazi kikamilifu ma hata katika wadi tuna wagonjwa 1800 wanaopokea matibabu kwa maradhi anuwai ” Daktari Kamuri alisema

Akielezea, Daktari Kamari akisema Kwamba Kuna mikakati Mingi inayowekwa na Serikali kuhakikisha Kwamba kila mkenya anapata huduma Bora ya Afya na kwa urahisi. Kamari aliongezea Kuwa wakianza huduma ya Afya ya UNC, changamoto nyingi zitashughulikiwa ikiwemo dawa na utunzaji Wa nyumbani.

READ ALSO:   This Is Amazing Business Of Raila Odinga's Youngest Son That's Winning Him Daily Bread

“Kuna mikakati mingi inayowekwa na serikali kuhakikisha kila Mkenya anapata huduma bora ya kiafya. Mara tu tutakapoanza Afya ya UHC, changamoto nyingi hizi zitashughulikiwa ikiwa ni pamoja na dawa na utunzaji wa nyumbani,” Daktari Kamari alisema

Wizara ya Afya nchini imetia mkazo kukabiliana na Janga la virusi Vya covid-19 huku huduma zingine zikisahauliwa kulingana na ripoti. Aidha, malalamiko ya hivi Punde yalisihi Serikali ikishirikiana na wizara ya Afya, kuhakikisha Kwamba inashughulikia magonjwa mengine na Wala si virusi Vya covid-19 peke yake.

Toa maoni, Shirikisha na Fuata Kwenye tovuti ya stateupdate.co.ke Kupokea Habari Zaidi

Advertisements
Advertisements

Leave a Reply

%d bloggers like this: