Connect with us

News

Hatimaye Mzozo Waibuka Miongoni Mwa Maseneta Kuhusu Mfumo Mpya Wa Ugamvi Wa Mapato

Lamech Bwabi

Published

on

Kidumbwedumbwe kilizidi kushamiri kwenye bunge la seneti baada ya maseneta kukubaliana kutokubaliana juu ya swala tata la ugamvi wa mapato.Kaunti zinazidi kupata pigo baada ya mjadala huu wa ugamvi wa mapato kwenye kaunti kuhairishwa kwa mara ya saba sasa.Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alitoa pendekezo hilo lililoungwa na wengi wa maseneta.
Kilingana na Murkomen, kuhairishwa kwa kikao hicho ni bora ili kiwape maseneta muda wa kutafuta njia mbadala ya kujadili hoja hii.Kwenye kikao cha hapo awali, pendekezo hili lilitolewa na kiranja wa wachache James Orengo lakini likapata pingamizi kutoka kwa maseneta 25 akiwamo Murkomen ambaye ameiunga mkono sasa.
Tume ya igamvi wa mapato CRA, ilikiwa imependekeza kuwa pesa zigawanywe kwenye kaunti kulingana na idadi ya watu.Mfumo huu mpya unahitaji mtu mmoja apewe shilingi moja kwa kuwa ana kura moja.Mfumo wa zamani ambao unapingwa vikali ulikiwa unagawa mapato kulingana na ukubwa wa eneo na si idadi ya watu.

Picha: Seneta Kipchumba Murkomen

Viongozi wakuu serikalini akiwemo Rais Kenyatta na Raila Odinga wameahindwa kushawishi maseneta kwenye mirengo yao kuunga mfumo huo mpya licha ya wao kuonyesha msimamo wao.Seneta wa Tharaka Nithi alitaka maseneta kuachiwa jukumu lao kuamua jinsi pesa hizo zitagawanywa maadamu wao ndio wanapigania ugatuzi.Raila alitangaza kuunga mfumo huo mpya.
Kaunti 19 zingepoteza shilingi hadi bilioni moja iwapo mfumo huo ungepitishwa na 28 zingepata nyongeza.Mingi ya kaunti kwenye maeneo ya pwani na mashariki yangeathirika nayo kwenye eneo la kati kuimarishwa.
Kabla ya kikao cha leo, madai yaliibuka kuwa maseneta walikuwa wanapewa milungula ili kupitisha hoja hiyo yenye utata.Kauli hii ilitolewa na seneta wa Narok Le Dama Ole Kina kupitia akaunti yake kwenye twitter.Seneta wa Nairobi Johstone Sakaja, pia wakati wa majadiliano aliibua madai kuwa ametishiwa iwapo hataunga mfumo huo mpya. Sakaja amedai kuwa imemlazimu wakati mwingine kulala mbali na kwake kutokana na maimamo wake wa kupinga hoja hiyo inayoungwa na chama chake.

Picha: Seneta Irungu Kang’ata

Aidha kiranja wa wengi kwenye seneti, Irungu Kang’ata amemkashifu vikali Sakaja kwa kukosa mkutano wa chama cha Jubilee ili kujadili swala hilo.Ikumbukwe kuwa hapo awali aliyekuwa naibu mwenye kiti wa Jubilee David Murathe alionya kuwachukulia hatua kali za kisheria maseneta waliopinga mfumo huo mpya. Baadhi ya maseneta lengwa ni Sakaja na Murkomen wanaopinga pendekezo hilo la kiranja wa wengi.

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Trending

%d bloggers like this: