Hatimaye Atakayemrithi Rais Kenyatta 2022 Abainika na Wala si Raila Odinga

0
1613851440348-46fd5ccc

Huku uchaguzi mkuu wa 2022 ukiwadia, hali ya sintofahamu yaibuka kwa Atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta anayetarajiwa kustaafu mnamo 2022. Rais Kenyatta ameongoza vipindi viwili mtawalia vinavyojumuisha miaka mitano kwa kila kipindi.

 

Rais Kenyatta na Naibu Wake William Ruto waling’oa nanga mnamo 2017 Katika Safari yao ya Urais Kama viongozi wateule huku wapinzani wao ikiwemo wa Karibu wa Chama Cha ODM Raila Odinga wakigonga mwamba.

 

 

Katika Kipindi Cha kwanza Cha wawili hawa uongozini, Upinzani umekuwa ukisuta Serikali ya Jubilee kwa Madai ya ufisadi na kutowashughulikia Wakenya ipasavyo.

Picha: Naibu Rais William Ruto akihutubia wananchi 

 

Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga na wenzake waliitaja Serikali ya Jubilee Kama fisadi na isiyo na mwongozo mwafaka kuendelenza Taifa la Kenya.

 

Aidha, huku sintofahamu ya Atakayemrithi Rais Kenyatta ikishika Kasi, taarifa zaibuka Kwamba Wenda Naibu rais William Ruto akawa mgombea mteule kumrithi Rais Kenyatta.

 

Taarifa zabaini kwamba Rais Kenyatta na Naibu Wake Ruto waliafikiana Katika Safari yao ya Urais nchini. Kulingana na maafikiano, Rais Kenyatta afaa kuongoza vipindi viwili mtawalia Kisha Naibu wake kumrithi kwa vipindi viwili.

 

Licha ya uungano baina ya Rais Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, taarifa zabaini kwamba wenda hali hiyo haitafaulu kuzamisha makubaliano hayo mwafaka.

READ ALSO:   Serikali Matatani Baada Ya Waathiriwa Wa Virusi Vya Corona Kutishia Kuandamana
Picha: Rais Kenyatta (kushoto) wakisalimiana na Kiongozi wa Upinzani Odinga(kuria)

 

Kutokana na Muungano huu uliozua majadiliano ya ujenzi wa madaraja yaani BBI, Naibu Rais William Ruto amekuwa akituhumiwa na kusutwa vikali na Wandani Wa Rais Kenyatta na Raila Odinga kwa minajili ya kuzamisha mpango wake wa kuwania urais mnamo 2022.

Aidha, taarifa zabaini kwamba Licha ya Upinzani huo, Ruto atawania Urais 2022 kufaulisha ndoto yake. Akihutubia hivi majuzi, Naibu rais alikariri Kwamba vitisho vya wapinzani wake wa kisiasa havitamzuia kuwania urais 2022 wala kulegeza kamba Katika safari yake ya kisiasa.

Fuata Kwenye tovuti stateupdate.co.ke Kupokea Habari zaidi.

Advertisements

Leave a Reply