Connect with us

Swahili News

Kilichosababisha Kifo Cha Magufuli Chabainika Na Wala Si Covid-19; Taarifa Zaibuka

Daniel Mutuva

Published

on

Picha: Rais Wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania Mwendazake John Pombe Joseph Magufuli

 

Huzuni watanda Katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na Kifo Cha Rais John Pombe Joseph Magufuli. Magufuli aliaga dunia mapema Jana majira ya saa kumi na mbili jioni akipokea matibabu Katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam. Magufuli amehudumu Kama Rais mteule wa Tanzania kwa vipindi viwili mtawalia ambapo alikuwa angali analiongoza kwa kipindi cha pili.

 

 

Akilihutubia taifa la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais nchini Samia Suluhu alibaini kwamba mwendazake Rais Mtukufu John Pombe Magufuli alitoweka Katika majira ya 6.00 jioni hapo jana akiwa anapokea matibabu katika hospitali ya Mzena jiji Dar es salaam, Tanzania.

 

 

Kulinga na taarifa zilizobainishwa na Makamu wa Rais Tanzania Bi Samia, Rais Magufuli alikuwa anakumbana na Tatizo la moyo na mfumo wa umeme, ugonjwa ambao amekuwa akikumbana nao zaidi ya miaka kumi.

 

Picha: Makamu wa Rais Wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu akihutubia taifa

 

Aidha, Mwendazake Magufuli alilazwa mnamo tarehe 6 Machi 2021 Katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Hali ilipozidi alipelekwa Katika hospitali ya Mzena Dar es salaam chini ya usimamizi wa tabibu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hadi Kifo chake kilichotokana na Tatizo la moyo na mfumo wa umeme.

READ ALSO:   Hofu Yatanda Baada Ya Msemaji Wa Serikali Kuambukizwa Homa Kali Ya Corona

 

Makamu wa Rais Samia Suluhu alikariri Kwamba kutakuwa na siku kumi na nne za maombolezi ambapo bendera zote zitawekwa nusu mlingoti kwa heshima za Mwendazake Rais Magufuli. Makamu wa Rais Samia alitangaza kwamba mipango ya mazishi itabainika hivi karibuni.

Fuata Kwenye tovuti www.stateupdate.co.ke Kupokea Habari zaidi

Advertisements
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Link Us In Facebook

Advertisement

Trending

%d bloggers like this: